KUTANA NA MFUNDISHAJI

Rahma Amer Mbarak

“Mtu anapokuwa na ujuzi kuhusu jambo fulani, unakuwa ni sehemu ya mtu huyo. Unakuwa sehemu ya mawazo ya mtu na mchakato wa ubunifu wake. Ujuzi unaongeza ubora wa mawazo na ubunifu wote wa baadaye wa mtu husika”- Ronald D. Davis.

Niliamua mwenyewe kuacha kuwa mwalimu na kuwa mwezeshaji wa watu wenye disleksia baada ya kusoma kitabu kinachoitwa “Gift of Dyslexia’ yaani ‘Kipaji cha Disleksia” kilichoandikwa na Ronald D. Davis. Kwa kufundisha miaka 6 nimekuwa na ujuzi kuhusu watoto lakini pamoja na upekee wa kila mtoto sikujifunza namna ya kuwafundisha kulingana na tofauti zao. Mpaka nilipoifahamu mbinu ya Davis™ ambayo imezibadili fikra zangu kabisa.

Disleksia mara nyingi haieleweki ipasavyo, huwa tunashughulikia tatizo kwa haraka na urahisi, bila kukubaliana na ukweli kwamba sisi wote ni tofauti na bila kukubali kutambua kipaji cha kuwa na disleksia na namna kinavyoweza kuwa na athari chanya kwa kiasi kikubwa. Kwa kuwa mwezeshaji wa kwanza kutoka Tanzania wa disleksia ninatarajia kurekebisha mitazamo na kusambaza elimu ya uelewa kuhusu kipaji cha mtu mwenye disleksia

UREKEBISHAJI

Urekebishaji katika program ya Davis Dyslexia ni mbinu ambayo inadhibiti matatizo ya vipaji vya ubongo ambavyo watu wenye disleksia wanakumbana nayo ili kutatua matatizo ya kujifunza. Kutokana na matatizo yao ya kutokuweza kutuchambua taarifa kwa kuona au kwa vitendo kama kwa kutumia mikono; mbinu ya Davis™ ya ufundishaji ni ya kuona na mbinu inayosisitiza kufahamu maana ambayo ni rahisi kwa mtu mwenye disleksia kujifunza. Programu imejikita katika kubadili mtazamo, kutoa msisitizo katika zana pamoja na ujuzi.

KUJIFUNZA KWA UBUNIFU

Mchakato wa kufikiri ni wa kutumia picha, mjifunzaji kufahamu maneno kupitia modeli ya 3D ambapo baadaye inakuwa sehemu ya mawazo yake.

ZANA BINAFSI ZA KUJISIMAMIA

Programu imejikita katika kubadili mtazamo, kufuatilia ari iliyo ndani ya mjifunzaji, kuzingatia zana na ufahamu.

TATIZO LA KUTOKUWA MZINGATIVU

Uelewa wa kina kuhusu maisha; kujidhibiti wakati baada ya kujua ni kwa nini.

KIPAJI

The Gift

KUFAHAMU KIPAJI

Kwa kila mmoja kumakinikia tatizo, sisi Davis tunaangalia kipaji cha kila mtu na kukiibua.

The Gift

UKUAJI

Kwa yote yanayoendelea katika ubongo wa mtu mwenye daileksia kwa kawaida ubongo wao unafanya kazi nyingi, kwa maneno na kuona, hivyo kushindwa kutambua mawazo wa picha nyingi kwa muda mchache. Tuanawapa fursa ya kufikiri na kupata mawazo, na kisha kupata dira ya watakachofikiri.

The Gift

FIKRA ZILIZOIMARISHWA

Ni zile zinazowawezesha kutafuta suluhisho kwa matatizo ya kitaalamu (kama Leonardo da Vinci) kuvumbua vitu vipya (kama Thomas Edison), kusimulia hadithi za kusisimua (kama Walt Disney) kujenga ujuzi usio wa kawaida kwa watu (kama Winston Churchill).

TATIZO

Kwa kawaida kusoma, kuandika na kutaja herufi ni jambo gumu na la kanganya. Hii inasababishwa na ukweli kwamba idadi kubwa ya maneno yana maana ambayo haiwezi kuoneshwa katika picha. Idadi hiyo inajumuisha maneno ya kawaida kwa mfano kama, na, au, pamoja na. Vivyo hivyo, pia namba na alama za hisabati zinaweza kukanganya. Kwa mfano kujua kwamba “tatu” inafanana na (3) haimaanishi kwamba mwanafunzi anajua ni alama inayowakilisha idadi ya (o o o). Mkanganyiko unaweza kuwa mkubwa kiasi kwamba mtu anashindwa :1). Kusoma 2).Kuandika 3). Kutaja herufi, 4). Kufanya hesabu, 5). Kusikiliza na kufahamu mwelekeo, 6) Kufanya mazungumzo ya kueleweka. Ni dhahiri kwamba hatuwezi kupata vipaji vyote hivi kwa kila mtu, lakini kama tukichunguza tutabaini kwamba kila mwenye matatizo ya kujifunza ana vipaji fulani maalumu. Kwa upimaji wa bure mtandaoni bonyeza hapa: Is it dyslexia?

VIPAJI VYA DAILEKSIA

Kwanini Davis?

Tunachotakiwa kufanya ni kuondoa mkanganyiko. Zana yetu ni ubunifu katika ujifunzaji binafsi. Kwa njia hii tunaweza kutengeneza picha za 3-D za maana za neno lolote au zana zinazokanganya, kwa kutumia njia ambayo inayohusisha ujifunzaji kwa kuona ambayo mtu mbunifu mara zote atakuwa huru nayo na kupata mafanikio kwa kuitumia.

1). Mbinu ya Davis™ ya kuwezesha wajifunzaji 2) Programu za Davis hufanya kazi pale ambapo nyingine zimeshindwa 3)Davis ni mbinu ya muda mfupi inayotoa mafanikio ya muda mrefu 4) Davis ni mbinu inayolenga uimarishaji 5)Davis inafaa kwa wajifunzaji wa rika zote 6) Davis inabadilikabadilika na inafurahisha 7).Davis inaweza kutumika katika lugha yoyote au mfumo wowote wa elimu.

SAFARI

Sikuweza kuvumilia, ilikuwa hainiingia akilini mwangu. Mtoto mmoja alikuwa amekaaa miongoni mwa wanafunzi wengine wa darasa la mwaka wa tatu. Niliwaangalia hao watoto ambao walikuwa na shauku na furaha ya kuianza siku. Aliniangalia sana. Ningekuwa nimeshasikia mengi kumuhusu mtoto huyu, mtoto mvivu! Kwa mwaka wote wa masomo siku zote alikuwa nyuma katika kuandika na kusoma. Hata hivyo, ulipofika wakati wa kujifunza kwa vitendo, kufanya shughuli za ubunifu wa mikono, kucheza mpira wa miguu alikuwa anaongoza. Hakuwa mvivu! Nikiwa na shauku ya kumsaidia, nilifanya utafiti na kusoma kuhusu daisleksia, nilipata cheti changu mtandaoni kuhusu watoto wenye matatizo ya kusoma na kuandika. Baada ya kupata cheti hicho nilielekezwa Programu ya Davis. Kuanzia hapo nimebadilika kutoka kuwa mwalimu na nimekuwa mwezeshaji. Ninafurahia kutumia uelewa na ufahamu wa vipaji vya wenye disleksia.

UNASWALI LOLOTE?

JISIKIE HURU KUWASILIANA NASI